انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · المرسلات
السورة ٧٧

المرسلات

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآيات ٢٥–٢٨

أَلَمْ نَجْعَلِ ٱلْأَرْضَ كِفَاتًا ٢٥ أَحْيَآءً وَأَمْوَٰتًا ٢٦ وَجَعَلْنَا فِيهَا رَوَٰسِىَ شَـٰمِخَـٰتٍ وَأَسْقَيْنَـٰكُم مَّآءً فُرَاتًا ٢٧ وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ ٢٨

{25 - 28} Yaani, kwani hakukuneemesheni kwa neema ya kuitiisha ardhi kwa masilahi yenu, tukaifanya "ardhi yenye kukusanya" nyinyi "Walio hai" majumbani "na maiti" makaburi. Kwa hivyo, kama vile majumba na makasri ni miongoni mwa neema za Mwenyezi Mungu juu ya waja wake, vile vile makaburi ni rehema kwao na kuwafunika miili yao inapooza ili wanyama vitu vinginevyo visiikaribie. "Na ndani yake tukaweka milima mirefu yenye kuthibiti" ili ardhi isiwayumbishe wakazi wake, basi Mwenyezi Mungu akaiweka imara kwa milima madhubuti na mirefu mipana "na tunakunywesheni maji matamu?" Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Je, mnayaona maji mnayoyanywa? Je, ni nyinyi mnayoyateremsha kutoka mawinguni au ni Sisi ndio wenye kuyateremsha? Tungelipenda, tungeliyafanya ya chumvi. Basi mbona hamshukuru?" Na akasema "Ole wao siku hiyo hao wanaokanusha" pamoja na yote aliyowaonyesha Mwenyezi Mungu miongoni mwa neema ambazo Yeye tu ndiye alizowaneemesha wao tu kwazo, lakini wakazikabili hizo kwa kukadhibisha.