المرسلات
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
أَلَمْ نَخْلُقكُّم مِّن مَّآءٍ مَّهِينٍ ٢٠ فَجَعَلْنَـٰهُ فِى قَرَارٍ مَّكِينٍ ٢١ إِلَىٰ قَدَرٍ مَّعْلُومٍ ٢٢ فَقَدَرْنَا فَنِعْمَ ٱلْقَـٰدِرُونَ ٢٣ وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ ٢٤
{20 - 24} Yaani, je, hatukukuumbeni, enyi wanadamu, "kwa maji ya kudharauliwa" yaliyotoka baina ya mifupa ya mgongo na mbavu, kisha Mwenyezi Mungu akayaweka "mahali pa utulivu madhubuti" ambapo ni tumbo la uzazi ambalo humo hukaa na kukua "Mpaka muda maalumu" uliowekwa na Mwenyezi Mungu. "Tukakadiria" na kumpangia mambo kijusi huyo katika viza hivyo, na tukakihamisha kutoka kwenye tone la manii ya kiume hadi kwenye kipande cha damu iliyogandana hadi kwenye pande la nyama mpaka Mwenyezi Mungu akakifanya kuwa mwili na akakipulizia roho ndani yake. Basi baadhi yao huufa kabla ya hapo "na Sisi ni wabora wa kukadiria." Kwani kukadiria kwake kufuata hekima yake na kunaendana na sifa zake. "Ole wao siku hiyo hao wanaokanusha" [baada ya Mwenyezi Mungu kuwabainishia Aya zake na kuwaonyesha mazingatio na hoja zilizo wazi].