انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الأنعام
السورة ٦

الأنعام

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٦١

وَهُوَ ٱلْقَاهِرُ فَوْقَ عِبَادِهِۦ ۖ وَيُرْسِلُ عَلَيْكُمْ حَفَظَةً حَتَّىٰٓ إِذَا جَآءَ أَحَدَكُمُ ٱلْمَوْتُ تَوَفَّتْهُ رُسُلُنَا وَهُمْ لَا يُفَرِّطُونَ ٦١

{61} "Na Yeye" mtukufu ni "Mwenye nguvu za kushinda juu ya waja wake." Kunatekelezeka kwao kutaka kwake kwa ujumla, na mapenzi yake ya ujumla, kwa hivyo wao hawana mamlaka yoyote juu ya jambo hili, na wala hawasongi wala hawatulii isipokuwa kwa idhini yake. Na licha ya haya, Amewawekea waja walinzi miongoni mwa Malaika wanaomlinda mja na wanamhifadhia yale aliyoyafanya. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Na hakika bila ya shaka wapo walinzi juu yenu. Waandishi wenye heshima. Wanayajua yale mnayoyatenda." "Wanaokaa kuliani na kushotoni. Hatamki neno lolote, isipokuwa karibu yake yupo mwangalizi aliye tayari;" basi huu ndio ulinzi wake kwao katika hali ya uhai; "mpaka mmoja wenu yakimjia mauti wajumbe wetu humfisha." Yaani, Malaika waliopewa jukumu ya kuchukua roho, "nao hawafanyi upungufu wowote" katika hilo. Basi hawaongezi hata saa moja katika yale aliyohukumu Mwenyezi Mungu na akajalia, wala hawapunguzi, wala hawatekelezi katika hilo isipokuwa kwa amri za Mwenyezi Mungu na mapitisho ya Mwenyezi Mungu.