الأنعام
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَهُوَ ٱلَّذِى يَتَوَفَّىٰكُم بِٱلَّيْلِ وَيَعْلَمُ مَا جَرَحْتُم بِٱلنَّهَارِ ثُمَّ يَبْعَثُكُمْ فِيهِ لِيُقْضَىٰٓ أَجَلٌ مُّسَمًّى ۖ ثُمَّ إِلَيْهِ مَرْجِعُكُمْ ثُمَّ يُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ٦٠
Yote haya ni uthibitisho wa uungu Wake, na ni hoja dhidi ya wale wanaomshirikisha Yeye, na ni ubainisho kwamba Yeye, Mtukufu ndiye anastahiki kupendwa, na ukuu, na heshima, na utukufu.
{60} Akajulisha kwamba Yeye peke yake ndiye Mwenye mwenye kuwaendesha waja wake katika hali yao ya kuwa macho, na katika kulala kwao, na kwamba Yeye huwafisha usiku kufisha kwa kulala. Kwa hivyo harakati zao zinatulia, na miili yao inastareheka, na huwaamsha katika usingizi wao. Ili watekeleze maslahi yao ya kidini na ya kidunia, na Mwenyezi Mungu Mtukufu anajua waliyofanya na kuchuma katika vitendo hivyo. Kisha yeye Mtukufu haachi kuwaendesha hivi mpaka watimize mida yao. Kwa hivyo anamaliza kwa kuendesha huku muda maalumu, nao ni muda wa maisha, na muda mwingine baada ya hapo, nao ni kufufuliwa baada ya kufa. Na ndiyo maana akasema, "kisha kwake Yeye ndiyo marejeo yenu;" si kwa mwingineye. "Kisha atawaambia yale mliyokuwa mkiyafanya;" ya heri na maovu.