انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الأنعام
السورة ٦

الأنعام

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٥٤

ثُمَّ ءَاتَيْنَا مُوسَى ٱلْكِتَـٰبَ تَمَامًا عَلَى ٱلَّذِىٓ أَحْسَنَ وَتَفْصِيلًا لِّكُلِّ شَىْءٍ وَهُدًى وَرَحْمَةً لَّعَلَّهُم بِلِقَآءِ رَبِّهِمْ يُؤْمِنُونَ ١٥٤

{154} Neno "Tena" katika nafasi hii, halikukusudiwa mpangilio wa matukio. Kwa maana zama za Musa, amani zimshukie, zilitangulia kusoma kwa Mtume Muhammad - rehema na amani ziwe juu yake - kitabu hiki. Na kilichokusudiwa ni mpangilio wa kutoa habari. Kwa hivyo, akajulisha kwamba alimpa "Musa Kitabu" ambacho ni Taurati "kwa kumtimizia" neema yake na ukamilifu wa ihsani yake, kwa "yule aliyefanya uzuri" katika umma wa Musa. Kwa maana, Mwenyezi Mungu aliwaneemesha wale wafanyao mazuri miongoni mwao kwa neema zisizodhibitika, ambazo miongoni mwake na utimilifu wake ni kuteremsha Taurati kwao. Basi ikatimia neema ya Mwenyezi Mungu juu yao, na ikawalazimu kuishukuru. "Na kuwa ni maelezo kina ya kila kitu" wanachohitaji kibainishwe, cha halali na haramu, na amri na makatazo, na itikadi na mfano wake, "na uwongofu na rehema." Yaani, inawaongoa kwenye heri, na inawajulisha shari katika misingi ya dini na matawi yake, "na rehema" ambayo kwayo wanapata furaha, na rehema, na heri nyingi; "ili" kwa sababu ya kukiteremsha kwetu Kitabu na hoja zilizo wazi kwao "waamini katika kukutana na Mola wao Mlezi." Kwani inajumuisha ushahidi mbalimbali wa uhakika juu ya kufufuliwa na malipo kwa matendo, [ambayo] yanawafanya kuamini katika kukutana na Mola wao Mlezi na kujiandaa kwa ajili ya hilo.