الأنعام
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَأَنَّ هَـٰذَا صِرَٰطِى مُسْتَقِيمًا فَٱتَّبِعُوهُ ۖ وَلَا تَتَّبِعُوا۟ ٱلسُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِۦ ۚ ذَٰلِكُمْ وَصَّىٰكُم بِهِۦ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ١٥٣
{153} Na alipobainisha nyingi katika amri kubwa na sheria muhimu, Akayaashiria na kwa kile kilicho cha jumla zaidi yake, kwa hivyo akasema: "Na kwamba hakika hii ndiyo Njia yangu iliyonyooka." Yaani, hukumu hizi na mfano wake miongoni mwa yale aliyoyabainisha Mwenyezi Mungu katika Kitabu chake na akayaweka wazi kwa waja wake ndio Njia ya Mwenyezi Mungu inayofikisha Kwake na kwenye nyumba ya utukufu wake, ambayo ni ya wastani, nyepesi, na fupi. "Basi ifuateni" ili mpate kufuzu na kufaulu, na mfikie matumaini na furaha mbalimbali, "Wala msifuate njia nyinginezo." Yaani, njia zinazohalifiana na Njia hii, "zikawafarikisha na Njia Yake;" yaani, zikawapoteza Njia hiyo, na zikawatawanya kulia na kushoto. Na mkipotea Njia hiyo iliyonyooka, basi hapo hakuna isipokuwa njia nyinginezo zinazofikisha katika Jahiim. "Haya amewausia ili mmche (Mwenyezi Mungu)." Kwani ikiwa mtafanya yale aliyowabainishia Mwenyezi Mungu kwa elimu na matendo, mtakuwa miongoni mwa Wachamungu, na waja wa Mwenyezi Mungu waliofaulu. Na Aliifanya Njia yake kuwa moja na akainasibisha naye Mwenyewe, kwa sababu ni njia moja tu inayofikisha Kwake, na Mwenyezi Mungu ndiye anayewasaidia wanafuata katika kuifuata.