انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الأنعام
السورة ٦

الأنعام

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٢٣

وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَا فِى كُلِّ قَرْيَةٍ أَكَـٰبِرَ مُجْرِمِيهَا لِيَمْكُرُوا۟ فِيهَا ۖ وَمَا يَمْكُرُونَ إِلَّا بِأَنفُسِهِمْ وَمَا يَشْعُرُونَ ١٢٣

{123} Na hawa ndio ambao wanatangantanga katika giza mbalimbali, na katika batili yao wanasitasita, na wala hawatoshani wote. Miongoni mwao wamo viongozi, na maraisi na wale wanaofuatwa, na miongoni mwao wapo wafuasi walio chini ya uongozi wao. Na wale wa kwanza miongoni mwao ndio wale walijishindia hali mbaya sana. Na kwa sababu hiyo akasema: "Na namna hivi tumeweka katika kila mji wakubwa wa wahalifu wake;" yaani viongozi ambao uhalifu wao umeshakuwa mkubwa, na upotofu wao ukawa mkali, "ili wafanye vitimbi ndani yake," kwa hadaa na kulingania kwenye njia ya Shetani na kupigana na Mitume na wafuasi wao kwa kauli na vitendo. Lakini vitimbi vyao na hila zao zinawarudia wao wenyewe, kwa sababu wanafanya vitimbi na Mwenyezi Mungu anafanya vitimbi, na Mwenyezi Mungu ndiye mbora zaidi wa wapangao vitimbi. Na kadhalika Mwenyezi Mungu huwafanya maimamu wakubwa wa uongofu na walio bora wao wapigane na wahalifu hawa na kuyakanusha maneno yao. Na wanapigana vita dhidi yao katika njia ya Mwenyezi Mungu, na wafuata kwa sababu ya hilo njia zinazowafikisha katika hilo, na Mwenyezi Mungu anawasaidia; na anaweka sawasawa rai yao, na anaiimarisha miguu yao, na anabadilisha siku baina za ushindi kati yao na maadui zao mpaka ilibadilishe jambo hili katika mwisho wake kwa kuwapa ushindi na kuwa kwao juu. Na mwisho mwema ni wa wachamungu.