الأنعام
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
أَوَمَن كَانَ مَيْتًا فَأَحْيَيْنَـٰهُ وَجَعَلْنَا لَهُۥ نُورًا يَمْشِى بِهِۦ فِى ٱلنَّاسِ كَمَن مَّثَلُهُۥ فِى ٱلظُّلُمَـٰتِ لَيْسَ بِخَارِجٍ مِّنْهَا ۚ كَذَٰلِكَ زُيِّنَ لِلْكَـٰفِرِينَ مَا كَانُوا۟ يَعْمَلُونَ ١٢٢
{122} Yeye Mtukufu Anasema: "Je, yule aliyekuwa" kabla ya Mwenyezi Mungu kumuongoa "maiti" katika giza mbalimbali ya ukafiri, na ujinga, na maasia, "kisha tukamhuisha" kwa nuru ya elimu, na imani, na utiifu. Kwa hivyo akawa anatembea miongoni mwa watu katika nuru, akiwa na utambuzi katika mambo yake, akiwa ameongoka kwenye njia yake, akiwa anajua heri, huku akiipendelea, akijitahidi katika kuitekeleza yeye mwenyewe na kwa wengine, huku akiujua uovu, akawa anauchukia, na anajitahidi katika kuuacha, na kuuondoa kutoka kwa nafsi yake mwenyewe na kutoka kwa wengine. Je, huyu ni sawa na yule aliye katika giza mbalimbali? Giza la ujinga, na upotovu, na ukafiri, na maasia, "sio wa kutoka humo," tayari njia zimemchanganyikia, na mahali pa kupitia pamemuwiya giza. Kwa hivyo akapatwa na wasiwasi mkubwa, na masikitiko, na huzuni na mashaka. Basi Yeye Mtukufu akazitanabahisha akili kwa yale zinayoyatambua, na kuyajua kwamba haya na haya hayawi sawa. Kama vile usiku na mchana haviwi sawa, na mwangaza na giza, na walio hai na wafu hawawi sawa. Na ni kama ilisemwa: Vipi atapendelea yule ambaye ana akili kidogo tu katika hali hii na kwamba abaki katika giza mbalimbali akiwa amechanganyikiwa? Kwa hivyo Akajibu: “makafiri wamepambiwa yale waliyokuwa wakiyafanya” kwa hivyo Shetani hakuacha kuwafanyia matendo yao kuonekena kuwa mazuri na kuwapambia hayo katika nyoyo zao mpaka wakayaona kuwa ni mazuri na wakayaona kuwa ndiyo haki. Na hayo yakawa ndiyo itikadi katika mioyo yao, na sifa madhubuti, yenye kutoachana nao. Kwa hivyo, waliridhika na yale waliyo juu yake ya uovu na mabaya.