انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الأنعام
السورة ٦

الأنعام

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١١٥

وَتَمَّتْ كَلِمَتُ رَبِّكَ صِدْقًا وَعَدْلًا ۚ لَّا مُبَدِّلَ لِكَلِمَـٰتِهِۦ ۚ وَهُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلْعَلِيمُ ١١٥

{115} Kisha akaeleza kwa kina, akasema, "Na yametimia maneno ya Mola Mlezi wako kwa ukweli na uadilifu;" yaani, ni ukweli katika kutoa habari, na uadilifu katika kuamirisha na kukataza. Kwa hivyo hakuna ya ukweli zaidi kuliko habari za Mwenyezi Mungu ambazo aliziweka katika Kitabu hiki kitukufu, wala hakuna la uadilifu zaidi ya maamrisho yake na makatazo yake. "Hakuna yeyote wa kuyabadilisha maneno yake." Kwa maana aliyahifadhi, na akayaweka sawasawa kwa aina ya juu zaidi ya ukweli, na ukomo wa haki. Bali haiwezekani kuyabadilisha wala kupendekeza kilicho bora zaidi yake. "Na Yeye ndiye Mwenye kusikia vyema" sauti zote kwa lugha mbali mbali, kwa aina zote za mahitaji. "Mwenye kujua yote" ambaye elimu yake imeyazunguka yote ya dhahiri na ya ndani, na yaliyopita na yajayo.