انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الأنعام
السورة ٦

الأنعام

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١١٤

أَفَغَيْرَ ٱللَّهِ أَبْتَغِى حَكَمًا وَهُوَ ٱلَّذِىٓ أَنزَلَ إِلَيْكُمُ ٱلْكِتَـٰبَ مُفَصَّلًا ۚ وَٱلَّذِينَ ءَاتَيْنَـٰهُمُ ٱلْكِتَـٰبَ يَعْلَمُونَ أَنَّهُۥ مُنَزَّلٌ مِّن رَّبِّكَ بِٱلْحَقِّ ۖ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ ٱلْمُمْتَرِينَ ١١٤

{114} Yani, sema, ewe Mtume, "Je, nimtafute hakimu asiyekuwa Mwenyezi Mungu?" Nitafute hukumu kutoka Kwake, na ninashikamana na amri zake na makatazo yake. Kwani asiyekuwa mwenyezi Mungu anahukumiwa yeye mwenyewe, si hakimu. Na kila uendeshaji mambo na hukumu ya viumbe vyote hivyo vinajumuisha upungufu, na kasoro, na dhuluma. Na hakika yule anayepasa kufanywa hakimu ni Yeye mwenyezi Mungu peke yake, asiyekuwa na mshirika yeyote, ambaye ana uumbaji na amri "ndiye aliyewateremshia Kitabu hiki kilichoelezwa kwa kina?" Yaani, ambacho ndani yake imewekwa wazi halali na haramu, na hukumu za kisharia, na misingi ya dini na matawi yake, ambayo hakuna ubainifu mkubwa zaidi kuliko ubainifu wake, na hakuna uthibitisho ulio bora zaidi kuliko uthibitisho wake, wala hakuna kilicho kizuri zaidi yake katika hukumu, wala hakuna kauli madhubuti zaidi kuiliko. Kwa sababu hukumu zake zinajumuisha hekima na rehema. na watu wa Vitabu vilivyotangulia, miongoni mwa Mayahudi na Manaswara wanakiri hilo, na "wanajua ya kwamba kimeteremshwa kutoka kwa Mola wako Mlezi kwa Haki." Na ndiyo maana habari zote zilikubaliana juu ya hilo "basi" kamwe usisitesite katika hayo wala "usiwe katika wale wanaotia shaka."