الأنعام
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
بَدِيعُ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ۖ أَنَّىٰ يَكُونُ لَهُۥ وَلَدٌ وَلَمْ تَكُن لَّهُۥ صَـٰحِبَةٌ ۖ وَخَلَقَ كُلَّ شَىْءٍ ۖ وَهُوَ بِكُلِّ شَىْءٍ عَلِيمٌ ١٠١
{101} "Yeye ndiye Muumbaji mwanzilishi wa mbingu na ardhi;" yaani, Muumba wa viwili hivyo, aliyeviunda vyema bila ya mfano wa kabla, kwa uumbaji mzuri zaidi na mpangilio, na uzuri, ambao akili za watu wenye akili timamu haziwezi kupendekeza chochote mfano wake, na wala hana mshirika yeyote katika kuumba kwa viwili hivyo. "Vipi awe na mwana, ilhali hakuwa na mke?" Yaani, vipi Mwenyezi Mungu atakuwa na mwana na ilhali Yeye ndiye Mungu, bwana mkusudiwa na wote ambaye hana mke? Naye hawahitaji viumbe wake, nao wote wanamhitaji Yeye, wanalazimika kutafuta msaada wake katika hali zao zote. Na mwana ni lazima awe kutoka katika aina moja na baba yake, na Mwenyezi Mungu ndiye Muumba wa kila kitu, na hakuna chochote katika kiumbe kinachofanana na mwenyezi Mungu kwa njia yoyote ile. Na alipotaja ujumla wa kuumba kwake vitu, Akataja elimu yake kuvienea. Kwa hivyo akasema, "Naye ndiye aliyeumba kila kitu. Naye ni Mwenye kujua vyema kila kitu." Na katika kuitaja elimu baada ya kuumba kuna ishara kwa ushahidi wa kiakili juu ya kuthibiti kwa elimu yake, nayo ni viumbe hivi na yale vinavyojumuisha ya mpangilio kamili, na uumbaji wa kimaajabu. Kwani katika hilo kuna ushahidi juu ya upana wa elimu ya Muumba wake, na ukamilifu wa hekima Yake. Kama alivyosema Yeye Mtukufu, "Kwa hajui yule aliyeumba, ilhali Yeye ndiye Mjua siri, Mwenye habari zote?" Na kama alivyosema Yeye Mtukufu, "Naye ndiye Muumbaji Mkuu, Mwenye kujua yote."