انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الأنعام
السورة ٦

الأنعام

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٠٠

وَجَعَلُوا۟ لِلَّهِ شُرَكَآءَ ٱلْجِنَّ وَخَلَقَهُمْ ۖ وَخَرَقُوا۟ لَهُۥ بَنِينَ وَبَنَـٰتٍۭ بِغَيْرِ عِلْمٍ ۚ سُبْحَـٰنَهُۥ وَتَعَـٰلَىٰ عَمَّا يَصِفُونَ ١٠٠

{100} Yeye Mtukufu anajulisha kwamba pamoja na ihsani yake kwa waja Wake, na kuwajulisha kwake Ishara Zake zilizo wazi na hoja zake zilizo wazi, kwamba wale wanaoshirikisha katika Maquraishi na wengineo walimfanyia Yeye washirika wanaowaomba na kuwaabudu miongoni mwa majini na Malaika, ambao ni viumbe miongoni mwa viumbe wa Mwenyezi Mungu, na ambao hawana sifa yoyote ya umola wala uungu. Lakini wao wakawafanya kuwa washirika kwa Yule aliye na uumbaji na amri, na Yeye ndiye anayeneemesha kwa kila aina ya neema, Mwenye kuzuia adhabu zote. Na tena washirikina walisingizia uongo na wakazua wao wenyewe kuwa Mwenyezi Mungu ana wana wa kiume na wana wa kike bila ya wao kuwa na elimu juu ya hilo. Na ni nani dhalimu zaidi kuliko yule anayemsingizia Mwenyezi Mungu bila ya kuwa na elimu, na akamzulia upungufu mbaya zaidi ambao ni lazima Mwenyezi Mungu atakaswe kutokana nao? Na kwa sababu hii, akajitakasa Mwenyewe kutokana na yale waliyomzulia washirikina, kwa hivyo akasema; "Yeye Ametakasika, na ametukuka juu ya hayo wanayomsifu kwayo!" Kwa maana Yeye Ametukuka huyo anayesifiwa kwa kila ukamilifu, na ametakasika kutokana na kila upungufu, na kasoro, na dosari.