الحشر
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
لَا يُقَـٰتِلُونَكُمْ جَمِيعًا إِلَّا فِى قُرًى مُّحَصَّنَةٍ أَوْ مِن وَرَآءِ جُدُرٍۭ ۚ بَأْسُهُم بَيْنَهُمْ شَدِيدٌ ۚ تَحْسَبُهُمْ جَمِيعًا وَقُلُوبُهُمْ شَتَّىٰ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَّا يَعْقِلُونَ ١٤
{14} “Hawatapigana nanyi kwa mkusanyiko.” Yaani, wakiwa wote pamoja, “isipokuwa katika vijiji vilivyoimarishwa kwa ngome, au nyuma ya kuta.” Yaani, hawatabaki imara katika kupigana nanyi, wala hawawezi kuazimia kufanya hivyo isipokuwa ikiwa watakuwa ndani ya ngome katika vijiji au nyuma ya kuta na ua. Hapo, huenda wanaweza kujizuia kwa kuzitegemea ngome hizo na kuta zao, si kwa sababu ya ushujaa wao wenyewe, na hili ni katika mambo makubwa yanayokashifiwa zaidi. “Wao kwa wao vita vyao ni vikali.” Yaani, hawana dosari katika miili yao wala nguvu zao, bali dosari yao iko katika udhaifu wa imani yao na ukosefu wa umoja katika neno lao. Ndiyo maana akasema: “Utawadhania kuwa wako pamoja” wakati unapowaona wakiwa pamoja, wakijionyesha hivyo “kumbe nyoyo zao ni mbali mbali.” Yaani, zinachukiana, zimetawanyika, na kutengana. “Hayo” yaliyowasababishia kusifika kwa hayo yaliyotajwa ni “kwa kuwa wao ni watu wasiotumia akili” kwani kama wangekuwa na akili, basi wangependelea kilicho bora kuliko kile ambacho si bora, na wala wasingejiridhia wenyewe kilicho duni kati ya mafungu haypo mawili, na neno lao lingekuwa moja, na nyoyo zao zingeungana. Na kwa hayo, wangeweza kusaidiana wao kwa wao, na wanashirikiana katika masilahi yao [na manufaa] yao ya kidini na ya kidunia. Basi mfano wa hao ndio wale walioachiliwa mbali katika Watu wa Kitabu, ambao Mwenyezi Mungu alimnusuru Mtume wake dhidi yao, na akawaonjesha hizaya katika maisha ya dunia, na kukosa msaada kutoka kwa wale waliowaahidi kuwasaidia.