انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الحشر
السورة ٥٩

الحشر

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٣

لَأَنتُمْ أَشَدُّ رَهْبَةً فِى صُدُورِهِم مِّنَ ٱللَّهِ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَّا يَفْقَهُونَ ١٣

{13} Na sababu iliyowapelekea kufanya hivyo ni kuwa nyinyi enyi Waumini “ni kitisho zaidi katika vifua vyao kuliko Mwenyezi Mungu.” Basi wakakuogopeni nyinyi zaidi kuliko wanavyomwogopa Mwenyezi Mungu, na wakatanguliza kumwogopa kiumbe ambaye haimilikii nafsi yake wala nafsi ya mwingine manufaa wala madhara mbele ya kumwogopa Muumba, ambaye mkononi mwake kuna madhara na manufaa, kupeana na kuzuilia. “Hayo ni kwa kuwa hao ni watu wasiofahamu kitu” katika daraja za mambo, na wala hawajui uhakika wa mambo, na wala hawafikirii matokeo yake. Na ufahamu wa kweli ni kutanguliza kumhofu Muumba, kumtumaini, kumpenda mbele ya wengineo, na kwamba hao wengineo mambo yao yanakuja nyuma ya mambo ya Mwenyezi Mungu.