انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · المائدة
السورة ٥

المائدة

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٥٦

وَمَن يَتَوَلَّ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ فَإِنَّ حِزْبَ ٱللَّهِ هُمُ ٱلْغَـٰلِبُونَ ٥٦

{56} Kisha akataja manufaa ya urafiki huu wandani, akasema, "Na mwenye kumfanya rafiki wandani Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wale walioamini, basi hakika kundi la Mwenyezi Mungu ndio wenye kushinda." Yaani, yeye ni katika kundi lililofungamanishwa na Mwenyezi Mungu kufungamanishwa kwa kumfanyia ibada na urafiki wandani, na kundi lake ndio washindi, ambao wana mwisho mwema katika dunia na Akhera. Kama alivyosema Yeye Mtukufu, "Na kwamba hakika jeshi letu ndio watakaoshinda." Na hii ni bishara kubwa kwa mwenye kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu na akawa katika kundi lake na jeshi lake kwamba ana ushindi. Hata kama utashindwa katika baadhi ya nyakati kwa sababu ya hekima ambayo Mwenyezi Mungu Mtukufu anataka, lakini mwisho wa jambo lake ni ushindi na nusura. Na ni nani mkweli zaidi katika kauli kuliko Mwenyezi Mungu?