غافر
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
هُوَ ٱلَّذِى خَلَقَكُم مِّن تُرَابٍ ثُمَّ مِن نُّطْفَةٍ ثُمَّ مِنْ عَلَقَةٍ ثُمَّ يُخْرِجُكُمْ طِفْلًا ثُمَّ لِتَبْلُغُوٓا۟ أَشُدَّكُمْ ثُمَّ لِتَكُونُوا۟ شُيُوخًا ۚ وَمِنكُم مَّن يُتَوَفَّىٰ مِن قَبْلُ ۖ وَلِتَبْلُغُوٓا۟ أَجَلًا مُّسَمًّى وَلَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ ٦٧
{67} Kisha ikathibitisha upweke wake huu kwamba Yeye ndiye Muumba wenu na Mtengenezaji wa maumbile yenu. Kwa hivyo, kama alivyokuumbeni peke yake, basi mwabuduni Yeye peke yake; akasema: "Yeye ndiye aliyewaumba kwa udongo." Na hilo lilikuwa kwa kuumba asili yenu na baba yenu Adam, amani iwe juu yake, "kisha kwa tone la manii." Huu ndio mwanzo wa kuumbwa kwa wanadamu wengineo waliobakia. Kwa hivyo akatanabaisha juu ya awamu zilizosalia kama vile pande la damu, kisha pande la nyama, kisha mifupa, kisha kupuliza roho. "Kisha akakutoeni katika hali ya mtoto mchanga, kisha" vivyo hivyo mkaendelea kuhama kutoka katika umbo alilowaumba Mwenyezi Mungu mpaka "mpate kufikilia utu uzima wenu," mkapata nguvu ya kiakili, kimwili na nguvu zake zinginezo zote za dhahiri na za ndani, "kisha mpate kuwa wazee. Na kati yenu wapo wanaokufa kabla" ya kufika utu uzima; "na ili mfikie muda uliokwisha wekwa" ambapo umri wenu unakuwa umeshaisha. "Na ili mpate kutumia akili" kuhusu hali zenu, mkajua kwamba aliyewakuza katika awamu hizi ana uwezo kamili na kwamba Yeye ndiye ambaye hakuna anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Yeye tu, na kwamba nyinyi mna upungufu katika namna zote.