انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · النساء
السورة ٤

النساء

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٩١

سَتَجِدُونَ ءَاخَرِينَ يُرِيدُونَ أَن يَأْمَنُوكُمْ وَيَأْمَنُوا۟ قَوْمَهُمْ كُلَّ مَا رُدُّوٓا۟ إِلَى ٱلْفِتْنَةِ أُرْكِسُوا۟ فِيهَا ۚ فَإِن لَّمْ يَعْتَزِلُوكُمْ وَيُلْقُوٓا۟ إِلَيْكُمُ ٱلسَّلَمَ وَيَكُفُّوٓا۟ أَيْدِيَهُمْ فَخُذُوهُمْ وَٱقْتُلُوهُمْ حَيْثُ ثَقِفْتُمُوهُمْ ۚ وَأُو۟لَـٰٓئِكُمْ جَعَلْنَا لَكُمْ عَلَيْهِمْ سُلْطَـٰنًا مُّبِينًا ٩١

{91} Kikundi cha tatu ni kaumu wanaotaka masilahi ya nafsi zao wenyewe bila kujali heshima yenu, nao ndio wale ambao Mwenyezi Mungu alisema juu yao. “Mtawakuta wengine” yani katika wanafiki hawa, “wanataka wapate salama kwenu” Yani kwa kuwahofu nyinyi, “na salama kwa watu wao. Kila wakirudishwa kwenye fitina, hudidimizwa humo.” Yani hawaachi kuendelea kuwa juu ya ukafiri wao na unafiki wao. Na kila kinapowatokea kitu miongoni mwa fitina zinazojitokeza, kinawapofusha na kuwadidimiza kwenye vichwa vyao, ukazidi ukafiri wao na unafiki wao. Na hawa kwa mwonekano ni kama kile kikundi cha pili, lakini kiuhalisia wao ni tofauti nalo. Kwani, kikundi cha pili waliacha kupigana na Waumini kwa sababu ya kuwaheshimu, si kwa kuziogopea nafsi zao. Na ama kundi hili, hao waliliacha hilo kwa sababu ya hofu, si kwa sababu ya heshima. Bali wangepata nafasi ya kupigana na Waumini, basi wangeiendea kuitumia. Kwa hivyo, hawa, ikiwa haitabainika kwao, na ikawa wazi uwazi mkubwa kujitenga kwao na Waumini, na kuacha kupigana nao, basi hao wanapigwa vita. Na ndiyo maana akasema, “Na ikiwa hawajitengi nanyi, na wakawaletea salama,” yani kufanya amani na makubaliano ya kutopigana, “na wakaizuia mikono yao, basi wakamateni na waueni popote mnapowakuta. Na hao, tumewapa nyinyi hoja zilizo wazi juu yao.” Kwa sababu wao wamepita mipaka, wenye kuwadhulumu nyinyi, wenye kuacha kufanya amani. Basi, wasilaumu isipokuwa nafsi zao wenyewe.