انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · النساء
السورة ٤

النساء

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٩٠

إِلَّا ٱلَّذِينَ يَصِلُونَ إِلَىٰ قَوْمٍۭ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَهُم مِّيثَـٰقٌ أَوْ جَآءُوكُمْ حَصِرَتْ صُدُورُهُمْ أَن يُقَـٰتِلُوكُمْ أَوْ يُقَـٰتِلُوا۟ قَوْمَهُمْ ۚ وَلَوْ شَآءَ ٱللَّهُ لَسَلَّطَهُمْ عَلَيْكُمْ فَلَقَـٰتَلُوكُمْ ۚ فَإِنِ ٱعْتَزَلُوكُمْ فَلَمْ يُقَـٰتِلُوكُمْ وَأَلْقَوْا۟ إِلَيْكُمُ ٱلسَّلَمَ فَمَا جَعَلَ ٱللَّهُ لَكُمْ عَلَيْهِمْ سَبِيلًا ٩٠

{90} Kisha Mwenyezi Mungu akayatoa makundi matatu katika kupigana vita na wanafiki hawa. Makundi mawili aliamrisha waachwe, na akakata amri katika hilo: Moja yake: Yule ambaye anafungamana na kaumu ambao baina yao na Waislamu kuna ahadi na agano la kuacha kupigana vita, kwa hivyo anajiunga nao, na anakuwa na hukumu yao katika kuhifadhi damu na mali. Na kikundi cha pili ni kaumu ambao “vifua vyao vina dhiki juu ya kupigana nanyi, au kupigana na kaumu yao.” Yani walibakia nafsi zao haziwezi kuruhusu kupigana na nyinyi wala kupigana na kaumu yao, na wakapenda kwamba waache kupigana na makundi mawili haya. Basi, hawa pia aliwaamrisha waachwe, na akataja hekima katika hilo kwa kauli yake, “Na lau angelipenda Mwenyezi Mungu, angeliwapa mamlaka juu yenu wangelipigana nanyi.” Kwa maana, mambo yanayowezekana ni ya makundi matatu: Ima wawe wako pamoja nanyi na wapigane na maadui zenu. Na hili ni gumu kwa watu hawa. Basi jambo likazunguka kati ya kupigana na nyinyi pamoja na kaumu yao, na kati ya kuacha kupigana vita na makundi haya mawili, ambayo ndilo rahisi zaidi katika mambo hayo mawili kwenu. Na Mwenyezi Mungu ana uwezo wa kuwapa mamlaka juu yenu. Kwa hivyo, kubalini salama, na mhimidini Mola wenu Mlezi ambaye aliizuia mikono yao kwenu pamoja na wao kuwa na uwezo juu ya hilo. Basi, hawa ikiwa watajitenga nanyi “na wasipigane nanyi, na wakawaletea amani, basi Mwenyezi Mungu hakuwapa nyinyi njia dhidi yao.”