الزمر
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
فَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن كَذَبَ عَلَى ٱللَّهِ وَكَذَّبَ بِٱلصِّدْقِ إِذْ جَآءَهُۥٓ ۚ أَلَيْسَ فِى جَهَنَّمَ مَثْوًى لِّلْكَـٰفِرِينَ ٣٢
{32} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema akionya na kutahadharisha kwamba hakuna dhalimu mkubwa zaidi "kuliko yule aliyemsingizia uwongo Mwenyezi Mungu." Ima kwa kumnasibisha na kile ambacho hakiufailii ukuu wake au kwa kudai unabii, au kwa kusema kwamba Mwenyezi Mungu alisema hivi au alijulisha hivi au alimhukumu hivi ilhali yeye ni mwongo katika hayo. Huyu imejumuishwa katika kauli yake Mtukufu: "Na kumsingizia Mwenyezi Mungu mambo msiyoyajua" ikiwa hajui, vinginevyo, basi hilo ni baya mno. Au "akaukadhibisha ukweli" ulioungwa mkono na ushahidi wa wazi "ulipomfikia" naye akaukadhibisha. Na ikiwa aliunganisha kati ya kumdanganyishia Mwenyezi Mungu na kukadhibisha ukweli, basi hiyo inakuwa dhuluma juu ya dhuluma." Je, siyo katika Jahannamu makazi ya hao makafiri," ambamo Mwenyezi Mungu atachukua haki kutoka kwa kila dhalimu na kafiri? "Kwani hakika ushirikina bila ya shaka ni dhuluma iliyo kubwa."