انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · ص
السورة ٣٨

ص

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٢٤

قَالَ لَقَدْ ظَلَمَكَ بِسُؤَالِ نَعْجَتِكَ إِلَىٰ نِعَاجِهِۦ ۖ وَإِنَّ كَثِيرًا مِّنَ ٱلْخُلَطَآءِ لَيَبْغِى بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ إِلَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ وَقَلِيلٌ مَّا هُمْ ۗ وَظَنَّ دَاوُۥدُ أَنَّمَا فَتَنَّـٰهُ فَٱسْتَغْفَرَ رَبَّهُۥ وَخَرَّ رَاكِعًا وَأَنَابَ ۩ ٢٤

{24} Daudi aliposikia maneno yake, akasema - na ilijulikana kutokana na muktadha wa maneno yake aliyosema hapo awali kwamba hayo ndiyo yaliyotokea hasa - kwa hivyo, hakuhitaji huyo mwengine kusema kitu, na hakuna msingi wowote kwa yule anayeweza kusema: 'Kwa nini Daudi alihukumu kabla ya kusikia maneno ya yule hasimu mwengine?' "Kweli amekudhulumu kwa kumtaka kondoo wako mmoja kuongezea kwenye kondoo wake." Hii ndiyo desturi ya wengi wanaochanganya vitu vyao. Na akasema: "Na hakika washirika wengi hudhulumiana wao kwa wao," kwa sababu dhuluma ni sifa ya nafsi zote "isipokuwa wale walioamini na wakatenda mema." Hao kuamini kwao na kutenda kwao mema kunawazuia kufanya dhuluma. "Na hao ni wachache," kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Ni wachache katika waja wangu ndio wanaoshukuru." "Na Daudi akajua," alipohukumu kati yao, "kuwa tumemfanyia mtihani" kwa kumletea tukio hili ili apate kutanabahi. "Basi akamwomba msamaha Mola wake Mlezi" kwa yale aliyoyafanya, "na akaanguka kusujudu na kutubia" kwa Mwenyezi Mungu, toba ya kweli na kumuabudu sawasawa.