انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · ص
السورة ٣٨

ص

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٢٣

إِنَّ هَـٰذَآ أَخِى لَهُۥ تِسْعٌ وَتِسْعُونَ نَعْجَةً وَلِىَ نَعْجَةٌ وَٰحِدَةٌ فَقَالَ أَكْفِلْنِيهَا وَعَزَّنِى فِى ٱلْخِطَابِ ٢٣

{23} Maana yake ni kwamba, ilijulikana mahasimu wawili hao walikuwa wamekusudia kufanyiwa haki iliyo wazi. Na ikiwa ndivyo hivyo, basi watamwambia habari zao kwa haki. Kwa hivyo, Nabii wa Mwenyezi Mungu, Daudi, hakuchukizwa na mawaidha waliyompa wala hakuwakemea kwa hilo. Mmoja wao akasema: "Hakika huyu ni ndugu yangu" katika dini, au ukoo, au urafiki kwa sababu hayo yanamzuia kunidhulumu, au kwa sababu udhalimu anaoweza kufanya ni mkubwa zaidi kuliko mtu mwingine, "ana kondoo wa kike tisini na tisa;" yaani, wa kike. Ambalo ni jambo linalomlazimu kuridhika na alichompa Mwenyezi Mungu. "Na mimi ninaye kondoo wa kike mmoja tu" lakini akamtamani. "Akasema: 'Nipe huyo nikufugie!' Na amenishinda kwa maneno." Na akaendelea hivyo mpaka akamchukua au akawa karibu mno kumchukua.