انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · يس
السورة ٣٦

يس

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٧٩

قُلْ يُحْيِيهَا ٱلَّذِىٓ أَنشَأَهَآ أَوَّلَ مَرَّةٍ ۖ وَهُوَ بِكُلِّ خَلْقٍ عَلِيمٌ ٧٩

{79} Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu akajibu kuona kwao huku kwamba haliwezekani kwa jawabu la kuponya, la kutosha.Akasema: "Sema: Ataihuisha huyo huyo aliyeiumba hapo mara ya mwanzo." Na hili, kwa kufikiria tu, anajua kwa yakini na bila ya shaka yoyote kwamba yule aliyeiumba mara ya kwanza ana uwezo wa kuirejesha mara ya pili, na hilo ndilo rahisi zaidi mbele ya uwezo ikiwa atafikiria vyema mwenye kufikiria. "Na Yeye ni Mjuzi wa kila kuumba." Huu pia ni ushahidi wa pili juu ya sifa za Mwenyezi Mungu Mtukufu. Nalo ni kwamba elimu yake, Mwenye nguvu, imewazunguka viumbe wake wote katika hali zao zote katika nyakati zote, na anajua ni nini ambacho ardhi inapunguza miongoni mwa miili ya wafu na ile iliyobakia, na anajua ghaibu na mambo ya dhahiri. Kwa hivyo, mja akiikiri elimu hii kubwa,atajua kwamba hilo ni kubwa zaidi na tukufu zaidi hata kuliko Mwenyezi Mungu kuwafufua wafu kutoka kwenye makaburi yao.