انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · يس
السورة ٣٦

يس

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٧٨

وَضَرَبَ لَنَا مَثَلًا وَنَسِىَ خَلْقَهُۥ ۖ قَالَ مَن يُحْىِ ٱلْعِظَـٰمَ وَهِىَ رَمِيمٌ ٧٨

{78} "Na akatupigia mfano" ambao haumfailii yeyote kuupiga. Nao ni kuufananisha uwezo wa Muumba na uwezo wa viumbe, na kwamba jambo lisilowezekana kwa uwezo wa viumbe pia haliwezekani kwa uwezo wa Muumba. Basi Mwenyezi Mungu akaufafanua mfano huu kwa kauli yake mwanadamu huyu. "Akasema:" Ni nani huyo atakayeihuisha mifupa nayo imekwishamung'unyika?" Huku ni kuuliza kwa njia ya kejeli. Huo ndio mchanganyiko wao na fikira yao potofu, nao huo ndio mfano aliotoa Mwenyezi Mungu. Na hilo ni kwamba jambo hili haliwezekani kabisa kulingana na jinsi wanavyojua wanadamu. Lakini kauli hii aliyosema mwanadamu huyu ni kauli iliyotokana na kughafilika kwake na kusahau mwanzo wa kuumbwa kwake. Lau kuwa angeufahamu vyema uumbaji wake baada ya kwamba hakuwa chochote cha kutajwa, kisha akafanywa kuwepo, akaonekana kwa macho, basi hangepinga mfano huu.