انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الروم
السورة ٣٠

الروم

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٢٠

وَمِنْ ءَايَـٰتِهِۦٓ أَنْ خَلَقَكُم مِّن تُرَابٍ ثُمَّ إِذَآ أَنتُم بَشَرٌ تَنتَشِرُونَ ٢٠

{20} Huu ndio mwanzo wa kuorodheshwa kwa ishara zake zinazoonyesha upekee wake katika uungu, ukamilifu wa ukuu wake, utekelezekaji wa mapenzi yake, na nguvu ya uweza wake, na uzuri wa matendo yake, na upana wa rehema yake na ihsani yake. Alisema, "Na katika Ishara zake ni kuwa aliwaumba kwa udongo" kwa kuumba asili ya dhuriya, Adam, amani iwe juu yake. "Kisha mmekuwa watu mliotawanyika kote kote." [Yaani, Yeye ndiye aliyewaumba nyinyi kutokana na asili moja na kiini kimoja], na akawaeneza katika pande mbalimbali za ardhi na sehemu zake. Katika hayo zimo ishara kwamba aliyewaumba kutokana na asili hii na akawaeneza katika pande zote za ardhi ndiye Mola Mlezi anayeabudiwa, Mfalme anayehimidiwa, Mwingi wa kurehemu, Mwingi wa mapenzi, ambaye atawarudisha kwa kuwafufua baada ya kufa kwenu.