انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · النمل
السورة ٢٧

النمل

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٧٨

إِنَّ رَبَّكَ يَقْضِى بَيْنَهُم بِحُكْمِهِۦ ۚ وَهُوَ ٱلْعَزِيزُ ٱلْعَلِيمُ ٧٨

{78} Yaani, Mwenyezi Mungu Mtukufu atatenganisha kati ya mahasimu hawa wawili na kuhukumu kati ya wale waliotofautiana kwa hukumu ya uadilifu na ya haki. Kwa hivyo, mambo yote, hata kama kuna mchanganyiko ndani yake katika dunia hii kati ya wale waliotofautiana kwa sababu ya ushahidi kufichika au kwa sababu ya makusudio fulani, Yeye hakika atabainisha haki inayoafikiana na hali halisi wakati Mwenyezi Mungu atatoa hukumu yake kuhusiana nayo. "Naye ni Mwenye nguvu" ambaye alishinda viumbe vyote, kwa hivyo wakamnyenyekea. "Ajuaye zaidi" kila kitu. Ajuaye zaidi maneno ya waliotofautiana, na kwa nini walitofautiana, na malengo na makusudi yao, na atamlipa kila mmoja wao kwa yale anayoyajua kumhusu.