انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · النمل
السورة ٢٧

النمل

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٤٢

فَلَمَّا جَآءَتْ قِيلَ أَهَـٰكَذَا عَرْشُكِ ۖ قَالَتْ كَأَنَّهُۥ هُوَ ۚ وَأُوتِينَا ٱلْعِلْمَ مِن قَبْلِهَا وَكُنَّا مُسْلِمِينَ ٤٢

{42} "Basi (Malkia) alipofika" akimjia Suleiman, alimwekea mbele kiti chake cha enzi, na alikuwa amekiona mara ya mwisho alipokuwa katika nchi yake, na "akaambiwa: Je, kiti chako cha enzi ni kama hiki?" Yaani, tunajua kwamba una kiti cha enzi kikubwa. Je, hicho ni kama kiti hiki tulichokuletea? "Akasema: Kama kwamba ndicho hiki." Na hili ni katika werevu wake na akili yake nzuri. Hakusema kwamba ndicho hicho; kwa sababu kilikuwa kimebadilishwa na kugeuzwa, na pia hakukataa kwamba si hicho; kwa sababu alikijua, kwa hivyo akatumia neno lenye maana hizo mbili, ambalo linaweza kutumika kwa hali mbili hizo. Suleiman akasema, akishangazwa na kuongoka kwake, na akili yake nzuri, huku akimshukuru Mwenyezi Mungu kwamba alimpa makuu kuliko aliyompa malikia "(Sulaiman na watu wake wakasema): Na sisi tumepewa elimu kabla yake (Malkia)." Yaani, uwongofu, na akili, na azimio, kabla ya malkia huyu, "na tukawa Waislamu" ambao ndio uwongofu wenye manufaa, wa kiasili. Na inawezekana kwamba hii ni katika maneno ya Malkia wa Sabai: Na tulipewa elimu kuhusu ufalme na mamlaka ya Suleiman, na wingi wa uwezo wake, kabla ya hali hii ambayo tuliona ndani yake uwezo wake wa kukileta kiti cha enzi kutoka mahali pa umbali mkubwa, kwa hivyo tukatii, na tukaja huku tumejisalimisha kwake, na kutii mamlaka yake.