انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · النمل
السورة ٢٧

النمل

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآيات ٣٢–٣٣

قَالَتْ يَـٰٓأَيُّهَا ٱلْمَلَؤُا۟ أَفْتُونِى فِىٓ أَمْرِى مَا كُنتُ قَاطِعَةً أَمْرًا حَتَّىٰ تَشْهَدُونِ ٣٢ قَالُوا۟ نَحْنُ أُو۟لُوا۟ قُوَّةٍ وَأُو۟لُوا۟ بَأْسٍ شَدِيدٍ وَٱلْأَمْرُ إِلَيْكِ فَٱنظُرِى مَاذَا تَأْمُرِينَ ٣٣

{32-33} Na katika azimio lake na akili yake nzuri ni kwamba aliwakusanya wakuu wa nchi yake na wanaume wa ufalme wake na akasema, "Enyi waheshimiwa! Nipeni shauri katika jambo langu hili;" yaani, niambie nini cha kumjibu? Je, tuingie chini ya utii wake na kufuata amri yake au tufanye nini? Yaani, kwani mimi sikati shauri yoyote bila ya rai zenu na ushauri wenu. "Wakasema: Sisi ni wenye nguvu na wakali kwa vita." Yaani, ikiwa utamjibu, na tusiingie chini ya utii wake, basi sisi hakika tuna nguvu ya kupigana nao. Na ni kana kwamba walielekea kwenye maoni haya, ambayo, ikiwa yangetimia, basi wangeangamizwa, lakini pia hawakutua juu ya maoni hayo, lakini walisema: "Na amri iko kwako" vile utakavyoona. Kwani walijua kwamba ni mwenye akili nyingi, na azimio kubwa, na mwenye kuwashauri vyema "basi tazama," kwa kufikiria na kuzingatia "ni nini unaamrisha."