انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · النمل
السورة ٢٧

النمل

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآيات ٢٩–٣١

قَالَتْ يَـٰٓأَيُّهَا ٱلْمَلَؤُا۟ إِنِّىٓ أُلْقِىَ إِلَىَّ كِتَـٰبٌ كَرِيمٌ ٢٩ إِنَّهُۥ مِن سُلَيْمَـٰنَ وَإِنَّهُۥ بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ ٣٠ أَلَّا تَعْلُوا۟ عَلَىَّ وَأْتُونِى مُسْلِمِينَ ٣١

{29-31} Basi akaenda nayo, akamtupia, kwa hivyo malkia huyo akawaambia watu wake, "Hakika nimeletewa barua tukufu" kutoka kwa mmoja wa wafalme wakubwa zaidi duniani, na kisha akaelezea yaliyomo ndani yake. Akasema: "Kwa hakika, imetoka kwa Suleiman nayo hakika ni: Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu. Msinifanyie jeuri, na fikeni kwangu nanyi mmekwisha kuwa wenye kusalimu amri." Na huu ni ufupisho mkubwa sana pamoja na kwamba imebainisha kwa ukamilifu; kwani ilijumuisha katazo lake la kumfanyia ujeuri, na kuendelea kudumu katika hali yao, na kwamba wafuate amri yake na waingie chini ya utiifu wake, na kwamba wamjie, na kuwalingania kwenye Uislamu. Pia ndani yake kuna pendekezo la kuanza kuandika kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu, na pia kuanza na jina la mwandishi mwanzoni mwa barua au andiko.