انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · النمل
السورة ٢٧

النمل

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٣

فَلَمَّا جَآءَتْهُمْ ءَايَـٰتُنَا مُبْصِرَةً قَالُوا۟ هَـٰذَا سِحْرٌ مُّبِينٌ ١٣

{13} Basi Musa, amani iwe juu yake, akaenda kwa Firauni na watu wake, na akawaita kwa Mwenyezi Mungu, na akawaonyesha ishara, "Basi zilipowafikia Ishara zetu hizo zenye kuonyesha" haki, na mtu anaona kwazo vyema kama vile macho yanavyoona kwa jua, "wakasema: Huu ni uchawi dhahiri." Na haikuwatosha kusema tu kwamba hayo ni uchawi, bali pia walisema: Ni (uchawi ulio) wazi na wa dhahiri kwa kila mtu! Na hili ni katika maajabu makubwa zaidi kwamba, ishara zenye kuonyesha na nuru zing'aazo kufanywa kuwa ndizo udanganyifu mkubwa na uchawi ulio wazi zaidi. Je, hili si isipokuwa katika kiburi kikubwa zaidi na ujanja wa kupindukia?