انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الفرقان
السورة ٢٥

الفرقان

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٦٩

يُضَـٰعَفْ لَهُ ٱلْعَذَابُ يَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ وَيَخْلُدْ فِيهِۦ مُهَانًا ٦٩

{69} Kisha akayafafanua kwa kauli yake, "Atazidishiwa adhabu Siku ya Qiyama, na atadumu humo" katika adhabu "kwa kufedheheshwa." Na tishio la kudumu humo ni kwa wale waliofanya yote hayo limethabiti bila shaka yoyote. Na pia kwa wale waliomshirikisha Mwenyezi Mungu. Na pia ahadi ya adhabu kali kwa kila moja ya haya matatu; kwa sababu hayo ima ni ushirikina au ni miongoni mwa dhambi kubwa zaidi. Na kudumu kwa muuaji na mzinzi katika adhabu, hao hawaingii katika hilo; kwa sababu maandiko ya Qur-ani na Sunna za Nabii yalionyesha kwamba waumini wote watatoka Motoni, na wala hatadumu humo Muumini yeyote, hata kama alifanya aliyofanya miongoni mwa maasia. Na Mwenyezi aliyataja matatu haya kwa sababu ndiyo dhambi kubwa zaidi. Kwa maana, ushirikina ndani yake kuna kuharibu dini, na mauaji ndani yake kuna kuharibu miili, na uzinzi ndani yake kuna kuharibu heshima.