الفرقان
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَٱلَّذِينَ لَا يَدْعُونَ مَعَ ٱللَّهِ إِلَـٰهًا ءَاخَرَ وَلَا يَقْتُلُونَ ٱلنَّفْسَ ٱلَّتِى حَرَّمَ ٱللَّهُ إِلَّا بِٱلْحَقِّ وَلَا يَزْنُونَ ۚ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ يَلْقَ أَثَامًا ٦٨
{68} "Na wale wasiomuomba mungu mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu" bali wanamwabudu Yeye peke yake, wakimkusudia Yeye tu dini yao, wanyoofu kwake bila ya kumtaka asiyekuwa Yeye. "Wala hawaui nafsi aliyoiharimisha Mwenyezi Mungu" Nayo ni nafsi ya Muislamu, na kafiri ambaye mwenye mkataba wa amani na Waislamu, "isipokuwa kwa haki." Kama vile kumua yule aliyeua mwingine, na kumuua mzinzi ambaye ameoleka, na kafiri ambaye anaruhusiwa kumuua. "Wala hawazini," bali wanazihifadhi tupu zao, isipokuwa kwa wake zao au kwa wale iliyowamiliki mikono yao ya kulia. "Na atakayefanya hayo;" yaani kumshirikisha Mwenyezi Mungu au kuua nafsi ambayo Mwenyezi Mungu ameharamisha bila ya haki au uzinzi, basi "atapata madhara."