انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الفرقان
السورة ٢٥

الفرقان

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآيات ٤٨–٤٩

وَهُوَ ٱلَّذِىٓ أَرْسَلَ ٱلرِّيَـٰحَ بُشْرًۢا بَيْنَ يَدَىْ رَحْمَتِهِۦ ۚ وَأَنزَلْنَا مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءً طَهُورًا ٤٨ لِّنُحْـِۧىَ بِهِۦ بَلْدَةً مَّيْتًا وَنُسْقِيَهُۥ مِمَّا خَلَقْنَآ أَنْعَـٰمًا وَأَنَاسِىَّ كَثِيرًا ٤٩

{48 - 49} Yaani, Yeye peke yake ndiye aliyewarehemu waja wake na akawapa riziki yake nyingi kwa kutuma pepo zenye bishara njema kabla ya rehema yake, ambayo ni mvua, kwa hivyo mawingu yakapeperushwa kwa hizo na kuunganishwa, na yakawa mapande mapande, kisha yakayapandisha na kuyajaza kwa idhini ya mwenye kuyaamrisha na kuyaendesha, ili waja wafurahie kwa mvua kabla ya kunyesha kwake, na ili wajitayarishe kwa ajili ya kabla kuwajia ghafla mara moja. "Na tunayateremsha kutoka mbinguni maji safi," yenye kusafisha kutokana na hadathi na maovu, na yanasafisha kutokana na udanganyifu na uchafu, na ndani yake kuna baraka miongoni mwa baraka zake. Nayo ni kwamba aliiteremsha ili ahuishe kwayo nchi uliyokufa, kisha ikaota humo aina mbalimbali za mimea na miti ambayo kwayo wanakula watu na wanyama "na tuwanyweshe wanyama na watu wengi tuliowaumba." Kwani je, si kweli kwamba yule aliyetuma pepo hizi zenye bishara njema na akazijalia kufanya matendo yake haya mbalimbali, na akateremsha maji safi kutoka mbinguni yenye baraka na riziki kwa waja na wanyama ndiye anayestahili kuabudiwa peke yake bila ya kushirikishwa na yeyote?