النور
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
لَّوْلَا جَآءُو عَلَيْهِ بِأَرْبَعَةِ شُهَدَآءَ ۚ فَإِذْ لَمْ يَأْتُوا۟ بِٱلشُّهَدَآءِ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ عِندَ ٱللَّهِ هُمُ ٱلْكَـٰذِبُونَ ١٣
{13} "Kwa nini hawakuleta mashahidi wanne?" Yaani, lau wale wasingizaji wangeleta mashahidi wanne dhidi ya yale waliyomsingizia. Yaani, waadilifu walioridhiwa. "Na ilivyokuwa, hawakuleta mashahidi wanne basi hao mbele ya Mwenyezi Mungu ni waongo;" hata kama walikuwa na yakini na hayo ndani yao wenyewe. Hakika wao ni waongo katika hukumu ya Mwenyezi Mungu, kwa sababu aliwakataza kusema juu ya hilo bila mashahidi wanne. Na ndiyo maana akasema, “Basi hao mbele ya Mwenyezi Mungu ni waongo.” Wala hakusema: Hao ni waongo. Na yote haya ni kwa ajili ya ukubwa wa utakatifu wa heshima na hadhi ya Muislamu. Kwa hivyo haijuzu kutangulia kuichafua kwa kuzulia uovu bila ya akidi ya ushahidi wa ukweli.