المؤمنون
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَهُوَ ٱلَّذِىٓ أَنشَأَ لَكُمُ ٱلسَّمْعَ وَٱلْأَبْصَـٰرَ وَٱلْأَفْـِٔدَةَ ۚ قَلِيلًا مَّا تَشْكُرُونَ ٧٨
{78} Mwenyezi Mungu Mtukufu anaeleza yale aliyowapa waja wake, akiwalingania kumshukuru na kutekeleza haki zake. Akasema: “Na ndiye aliyewaumbia kusikio” ili kwa hayo mpate kuyajua yanayosikika na kunufaika katika nafsi zenu, dini yenu na maisha yenu ya kidunia. “Na macho;” ili mpate kuyaona yanayoonekana na mpate kufaidika nayo kwa maslahi yenu, “na nyoyo.” Yaani, akili ambayo kwamba mnapata kujua nayo vitu na mnatofautika kwayo kutoka kwa wanyama. Basi lau mngelikosa masikio na macho na akili kwamba mngelikuwa viziwi na vipofu na bubu; ingelikuwaje hali yenu? Je, mnapoteza nini katika mahitaji yenu na ukamilifu wenu? Basi je, hamumshukuru yule aliyekufanyieni hisani kwa neema hizi; basi mkasimama katika kumpwekesha na kumtii? Lakini kushukuru kwenu ni kudogo, pamoja na mfululizo wa neema juu yenu.