انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · المؤمنون
السورة ٢٣

المؤمنون

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٦٨

أَفَلَمْ يَدَّبَّرُوا۟ ٱلْقَوْلَ أَمْ جَآءَهُم مَّا لَمْ يَأْتِ ءَابَآءَهُمُ ٱلْأَوَّلِينَ ٦٨

{68} "Je, hawakuifikiri kauli?" Yaani, je, hawaitafakari Qur-ani, na wakaizingatia na wakaifikiri; yaani, kama wao wangeliizingatia; ingeliwawajibishia imani , na ingeliwazuia wasikufuru, bali msiba uliowapata ni kwa sababu ya kukataa kwao kufanya hivyo. Hii ilionyesha kwamba, kutafakari kwa Qur-ani kunaita katika mema yote na kukataza dhidi ya maovu yote, na lilowazuia kuitafakari Qur-ani ni kwamba, mioyo yao ina kufuli. "Au yamewajia yasiyowafikia baba zao wa zamani?" Yaani, walizuiwa kuamini kwamba aliwajia mjumbe na kitabu ambacho hakikuwafikia baba zao wa zamani, walijifaridhishia kufuata njia ya baba zao waliopotea, na wakapinga kila kitu ambacho kilikuwa kinyume na hayo! Kwa sababu hiyo, wao na makafiri wengine kama wao walisema juu ya aliyowaambia Mwenyezi Mungu: "Na kadhalika hatukumtuma kabla yako mwonyaji kwenye mji wowote ila watu wake waliodeka kwa starehe walisema: 'Hakika sisi tuliwakuta baba zetu wanashika dini makhsusi, na sisi tunafuata nyayo zao.' Na Mwenyezi Mungu aliwajibu kwa kauli yake, "Akasema: Nikiwajieni na mwongozo bora kuliko yale mliyowapata baba zenu juu yake je, mtanifuata," ikiwa makusidio yenu ni haki? Walijibu kwa uhakika wa hali yao, "Walisema, Hakika sisi tunayakataa hayo mliyotumwa nayo."