انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · المؤمنون
السورة ٢٣

المؤمنون

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٦٧

مُسْتَكْبِرِينَ بِهِۦ سَـٰمِرًا تَهْجُرُونَ ٦٧

{67} "Na huku mkiitakabari na usiku mkiizungumza (Quran) kwa dharau." Walisema wafasiri, maana yake; wanatakabari ina kwenye nyumba ya kawaida ya wanaoongea au Al-haram (mahali patakatifu). Yaani, wanatakabari kwa watu kwa sababu yake. Wanasema: Sisi ni watu wa Al-haram; sisi ni bora kuliko wengine na wenye daraja ya juu. "Usiku mkiizungumza (Qur-ani);" yaani, kundi la watu wanaoizungumza usiku karibu na nyumba, "kwa dharau." Yaani, mnasema maneno ya dharau ambayo ni ya kuchukiza katika Qur-ani hii; wakanushaji ilikuwa njia yao katika hii Qur-ani ni kuikataa na kujitenga nayo, na baadhi yao wakiwahusia wengine wao kwa hilo. "Na walio kufuru walisema: Msiisikilize Qur-ani hii, na tumieni zogo, huenda mkashinda." Na akasema Mwenyezi Mungu juu yao:"Je, mnayastaajabia maneno haya? Na mnacheka, wala hamlii? Nanyi mmeghafilika?" "Au ndio wanasema: Ameitunga hii!" Walipokuwa wanajikusanya katika kufanya uovu huu; hapana shaka ilistahiki juu yao adhabu, na ilipotokea juu yao adhabu; hawakuwa naye wa kuwanusuru wao, wala mwokozi wa kuwaokoa wao,na wanakemewa juu ya hilo kwa vitendo hivi viovu.