المؤمنون
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَأَنزَلْنَا مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءًۢ بِقَدَرٍ فَأَسْكَنَّـٰهُ فِى ٱلْأَرْضِ ۖ وَإِنَّا عَلَىٰ ذَهَابٍۭ بِهِۦ لَقَـٰدِرُونَ ١٨
{18} "Na tumeteremsha kutoka mbinguni maji," ili yawe riziki kwa yenu na ya wanyama wenu kwa kiasi kinachowatosha, na wala haipunguzi [kwa namna ambayo haiwezi kuitosha ardhi na miti, kwa hivyo kikawa hakipatikani kile kilichokusudiwa nayo. Na tena haizidishi kwa kiasi ambacho haiwezi kustahimili], mpaka ikaharibu makazi, na wala mimea na miti ikawa haiwezi kumea humo. Bali anaishusha wakati inapohitajika kushuka, kisha akaiondoa wakati kunapokuwa kuendelea kwake ni madhara, "tukayatuliza katika ardhi" na akatoa jozi zote za mimea yule aliyeyashusha, tena akayafanya kukaa tayari ndani yake hazina ya ardhi, kwa namna ambayo hayakuendelea kushuka hadi yasifikiwe wala isifikiwe sehemu yake ya chini zaidi. "Na hakika Sisi tunaweza kuyaondoa. " Ima kwa kutoyateremsha, au huyateremsha kisha yakadidimia ndani kiwango cha kutofikiwa, au yasifikiwe makusudio yake. Na hii ni tanabahisho lake kwa waja wake kwamba wamshukuru kwa neema yake na wapime lau kuwa haingekuwa, ni madhara gani yangewapata. Kama vile kauli yake, "Sema, mwaonaje, ikiwa maji yenu yatadidimia chini, ni nani atakayewaletea maji yanayomiminika?"