الحج
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَلَا يَزَالُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ فِى مِرْيَةٍ مِّنْهُ حَتَّىٰ تَأْتِيَهُمُ ٱلسَّاعَةُ بَغْتَةً أَوْ يَأْتِيَهُمْ عَذَابُ يَوْمٍ عَقِيمٍ ٥٥
{55} Mwenyezi Mungu Mtukufu anatuambia kuhusu hali ya makafiri, na kwamba bado wana shaka juu ya uliyowaletea, ewe Muhammad. Kwa sababu ya ukaidi wao na kukengeuka kwao, na kwamba wataendelea kuwa katika hali hii, "mpaka Saa ya Kiyama iwafikie kwa ghafla." Yaani: kwa mshangao, "au iwajiye wao adhabu ya Siku Tasa." Yaani, hakuna kheri ndani yake, nayo ni Siku ya Kiyama. Basi ikiwafikia Saa ya Kiyama au ikawajia siku hiyo; waliokufuru watajua kuwa wao walikuwa ni waongo, na wakajuta pale ambapo majuto hayatawafaa, na wakadanganyika na kunyimwa wema wote, na wakatamani wangemuamini Mtume na wakafuata njia pamoja naye. Katika hili lipo onyo dhidi yao wanaoishi katika ukafiri wao na ufisadi wao.