طه
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَإِن تَجْهَرْ بِٱلْقَوْلِ فَإِنَّهُۥ يَعْلَمُ ٱلسِّرَّ وَأَخْفَى ٧
{7}"Na ukinyanyua sauti kwa kusema, basi hakika Yeye anajua siri na chini zaidi kuliko siri," miongoni mwa yale yaliyo ndani ya mioyo na ambayo hakuyatamka. Au siri ni yale yaliyomo moyoni, nayo yaliyoficha zaidi ya siri ni yale ambayo hata hayajatokea moyoni bado. Yeye Mwenyezi Mungu mtukufu anajua kwamba hayo yatakuja fika moyoni mwake katika wakati wake na kwa namna fulani. Na maana ya haya ni kwamba elimu yake imevizunguka vitu vyote, vidogo mno vyake na vikubwa vyake, vifiche vyake na vya dhahiri vyake. Basi ni sawa ukinyanyua sauti yako au ukaisema kwa siri. Hayo yote ni sawa kwa mujibu wa elimu yake Yeye Mtukufu.