انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · طه
السورة ٢٠

طه

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٢٥

قَالَ رَبِّ ٱشْرَحْ لِى صَدْرِى ٢٥

{25} Basi hapo Musa, amani iwe juu yake, akajua kwamba amebeba mzigo mkubwa. Ambapo alitumwa kwa dhalimu huyu mkaidi, ambaye hana mshindani yeyote huko Misri miongoni mwa viumbe, na Musa, amani iwe juu yuko peke yake, na tena alikuwa amefanya aliyofanya ya kumuua (Mmisri). Kwa hivyo, akatekeleza amri ya Mola wake Mlezi, na akaipokea kwa moyo mkunjufu na kuikubali, na akamuomba msaada na kumrahisishia njia ambazo ni sehemu ya ukamilifu wa ulinganizi wake, akasema, "Ewe Mola wangu Mlezi! Nikunjulie kifua changu" ili niweze kubeba madhara ya kimaneno na ya kivitendo, na wala moyo wangu usihuzunike kwa sababu ya hayo, wala kifua changu kisipate dhiki. Kwa maana kifua kinapokuwa na dhiki, mwenyewe hafailii kuwa muongoze wa viumbe na kuwalingania. Mwenyezi Mungu alimwambia Nabii wake Muhammad- rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, “Basi ni kwa sababu ya rehema itokayo kwa Mwenyezi Mungu ndiyo umekuwa laini kwao. Na lau ungelikuwa mkali, mwenye moyo mgumu, bila ya shaka wangelikukimbia.” Na pengine viumbe watakubali haki wanapoamiliwa kwa ulaini, upana na ukunjufu wa kifua.