البقرة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
أَلَآ إِنَّهُمْ هُمُ ٱلْمُفْسِدُونَ وَلَـٰكِن لَّا يَشْعُرُونَ ١٢
(12) “Hakika wao ndio waharibifu." Kwa maana, hakuna mharibifu mkubwa zaidi kuliko mwenye kukufuru (kukataa) aya (ishara) za Mwenyezi Mungu, na akazuia njia ya Mwenyezi Mungu. Na akamhadaa Mwenyezi Mungu na vipenzi wake, na akawategemea wale wanaompiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na akadai pamoja na hayo kuwa huko ni kutengeneza. Basi je, baada ya uharibifu huu kuna uharibifu mwingine? Lakini wao hawajui elimu ya kuwanufaisha, ingawa walikwisha jua elimu ambayo kwayo hoja ya Mwenyezi Mungu ilisimama juu yao. Na kulikuwa kutenda [maasia] katika ardhi uharibifu kwa kuwa ndiyo sababu ya kuharibika kwa yale yaliyopo juu ya uso wa ardhi kama vile nafaka, matunda, miti, na mimea, kwa sababu ya ule uharibifu unaovipata kwa sababu ya maasia. Na kwa sababu kutengeneza mambo katika ardhi ni kuiimarisha kwa kumtii Mwenyezi Mungu na kumwamini. Hii ni kwa sababu, Mwenyezi Mungu aliwaumba viumbe na akawafanya kuishi katika ardhi, na akawapa riziki ili wajisaidie kwayo katika kumtii na kumuabudu. Kwa hivyo, yakifanyika humo kinyume chake, basi hilo litakuwa kuwania kufanya uharibifu (ufisadi) ndani yake na kuibomoa, tofauti na ilichoumbwa (ardhi) kwa ajili yake.