انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · البقرة
السورة ٢

البقرة

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١١

وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ لَا تُفْسِدُوا۟ فِى ٱلْأَرْضِ قَالُوٓا۟ إِنَّمَا نَحْنُ مُصْلِحُونَ ١١

(11) Yaani, wanapokatazwa hawa wanafiki kufanya uharibifu katika ardhi, nao ni kufanya ukafiri na maasia, miongoni mwake ni kufichua siri za Waumini kwa adui wao na kuwategemea makafiri, “wanasema: Bali sisi ni watengenezaji;” basi wakachanganya baina ya kufanya ufisadi katika ardhi na kuonyesha kwamba huo sio ufisadi, bali ni utengenezaji ili kugeuza uhakika. Na kuchanganya kati ya kufanya batili na kuitakidi kuwa ndio haki; na hao wanafanya dhambi kubwa mno kuliko anayetenda maasia pamoja na kuitakidi uharamu wake. Huyu yuko karibu zaidi na usalama, na anatarajiwa zaidi kwamba atarudi. Na pindi ilipokuwa katika kusema kwao “Bali sisi ni watengenezaji," kuzuilia utengenezaji upande wao tu – ambako (huko kuzuilia) kunamaanisha kuwa Waumini sio miongoni mwa watu wanaotengeneza - Mwenyezi Mungu aliwageuzia madai yao hayo kwa kauli yake: