انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · مريم
السورة ١٩

مريم

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٤٣

يَـٰٓأَبَتِ إِنِّى قَدْ جَآءَنِى مِنَ ٱلْعِلْمِ مَا لَمْ يَأْتِكَ فَٱتَّبِعْنِىٓ أَهْدِكَ صِرَٰطًا سَوِيًّا ٤٣

{43} "Ewe baba yangu, kwa yakini imenifikia elimu ambayo haikukujia wewe." Yaani, ewe baba yangu, usinidharau na kusema: Mimi ni mwanao, nawe unacho kitu nisichokuwa nacho. Bali Mwenyezi Mungu amenipa elimu ambayo hakukupa wewe. Maana ya hilo ni kauli yake, "Basi nifuate mimi, nami nitakuongoza njia sawa." Yaani, njia iliyonyooka, ya wastani. Ambayo ni kumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake, bila ya mshirika yeyote, na kumtii yeye katika kila hali. Na katika maneno yake haya kuna kumuongelesha baba yake kwa njia nzuri ya upole na ulaini ambako hakufichiki. Kwa maana hakusema, 'Ewe baba yangu, mimi nina elimu ilhali wewe ni mjinga;' au 'Wewe huna elimu yoyote.' Bali alitumia njia yenye [kulazimu] kwamba mimi nina elimu na wewe pia una elimu, na ya kwamba elimu iliyonifikia haikukufikia wewe wala haikukujia. Kwa hivyo, unapaswa kufuata hoja na kujisalimisha kwayo.