انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · مريم
السورة ١٩

مريم

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٤٢

إِذْ قَالَ لِأَبِيهِ يَـٰٓأَبَتِ لِمَ تَعْبُدُ مَا لَا يَسْمَعُ وَلَا يُبْصِرُ وَلَا يُغْنِى عَنكَ شَيْـًٔا ٤٢

{42} Na Mwenyezi Mungu alitaja namna alivyokuwa anamrai, akasema, "Alipomwambia baba yake" akimwonyesha ubaya wa kuabudu masanamu: "Ewe baba yangu! Kwa nini unaabudu visivyosikia, na visivyoona, na visivyokufaa chochote?" Yaani, kwa nini unaabudu masanamu ambayo yana upungufu wao wenyewe na hata katika matendo yao. Hawasikii, hawaoni, na hawana uwezo wa kumnufaisha mwenye kuwaabudu wala kumdhuru. Bali wao wenyewe hawajimilikii manufaa yoyote, wala hawawezi kuzuia chochote? Huu ni uthibitisho wa wazi unaoonyesha kwamba kuabudu kilicho kipungufu chenyewe na ni kipungufu pia katika vitendo vyake ni jambo baya katika akili na sheria. Na maonyo yake Ibrahim na ishara yake vikaonyesha kuwa anayepaswa kuabudiwa na ambaye ni vizuri kumfanyia hivyo ni yule ambaye ana ukamilifu. Ambaye hakuna neema yoyote inayowafikia waja isipokuwa kutoka kwake, wala hakuna anayewazuilia adhabu isipokuwa Yeye tu. Naye ni Mwenyezi Mungu Mtukufu.