الكهف
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَتَرَكْنَا بَعْضَهُمْ يَوْمَئِذٍ يَمُوجُ فِى بَعْضٍ ۖ وَنُفِخَ فِى ٱلصُّورِ فَجَمَعْنَـٰهُمْ جَمْعًا ٩٩
{99} Inawezekana kwamba neno "tutawaacha" linamaanisha Yaajuju na Maajuju, na kwamba watakapowatokea watu, kwa sababu ya wingi wao na kujaa kwao katika ardhi yote, wachanganyike wao kwa wao. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Hata watakapofunguliwa Yaajuju na Maajuju wakawa wanateremka kutoka kila mlima.'' Na inawezekana kwamba neno "tutawaacha" linawarudia viumbe wote Siku ya Qiyama, na kwamba watakusanyika ndani yake, na wawe wengi, na wasonganesongane wao kwa wao kwa sababu ya uzito na dhiki na mitetemeko mikubwa. Kwa ushahidi wa kauli yake:
{99} Yaani, Israfil atakapolipuliza katika baragumu, Mwenyezi Mungu atazirudisha roho zote katika viwiliwili, kisha atawakusanya katika pahali pa kusimama katika Siku ya Qiyama. Atawakusanya wa kwanza katika wao na wa mwisho, makafiri na waumini ili waulizwe, na wahesabiwe, na walipwe kwa matendo yao.