انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الإسراء
السورة ١٧

الإسراء

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٨٢

وَنُنَزِّلُ مِنَ ٱلْقُرْءَانِ مَا هُوَ شِفَآءٌ وَرَحْمَةٌ لِّلْمُؤْمِنِينَ ۙ وَلَا يَزِيدُ ٱلظَّـٰلِمِينَ إِلَّا خَسَارًا ٨٢

{82} Qur-ani inajumuisha uponyaji na rehema, lakini hilo si kwa kila mmoja. Bali ni kwa wale wanaoiamini na kusadiki ishara zake na kuzijua. Na ama madhalimu ambao hawaiamini au hawaifanyi kazi, basi Aya zake haziwazidishi isipokuwa hasara tu. Kwa sababu, kwazo hoja inasimama juu yao. Kwa hivyo, uponyaji ambao Qur-ani imeujumuisha ndani yake ni jumla kwa ajili ya kuponya nyoyo kutokana na fikira potofu, ujinga, maoni potovu, ukengeufu mbaya, na nia mbaya. Kwa maana, inajumuisha elimu ya yakini ambayo kwayo zinaisha kila fikira potofu na ujinga, na yanapatikana mawaidha na ukumbusho ambao kwa hayo yanaisha kila matamanio yanayohalifu amri ya Mwenyezi Mungu. Nayo pia ina uponyaji wa miili kutokana na maumivu yake na maradhi yake. Na ama rehema, kutokana na sababu na njia ambazo inazihimiza, kila wakati mja anapozifanya, anapata rehema, furaha ya milele, na malipo ya haraka na ya baadaye.