الإسراء
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَرَبُّكَ أَعْلَمُ بِمَن فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ۗ وَلَقَدْ فَضَّلْنَا بَعْضَ ٱلنَّبِيِّـۧنَ عَلَىٰ بَعْضٍ ۖ وَءَاتَيْنَا دَاوُۥدَ زَبُورًا ٥٥
{55} "Na Mola wako Mlezi anawajua vilivyo waliomo mbinguni na katika ardhi" miongoni mwa kila aina ya viumbe, basi humpa kila mmoja wao anachostahiki na kinachohitajiwa na hekima yake, na huwafadhilisha baadhi yao kuliko wengine katika sifa zote za kihisia na zisizo za kihisia. Kama vile alivyowafadhilisha baadhi ya Manabii walioshiriki katika ufunuo wake juu ya wengine kwa fadhila na sifa mbalimbali kutokana na yale aliyowaneemesha kwayo miongoni mwa sifa za kusifiwa, tabia za kuridhisha, matendo mema, idadi kubwa ya wafuasi, na baadhi yao kuteremshiwa vitabu vilivyo na hukumu za kisheria na itikadi zinazoridhiwa, kama alivyomteremsha Daudi Zaburi. Nacho ni kitabu kinachojulikana sana. Na ikiwa Mwenyezi Mungu Mtukufu amefadhilisha baadhi yao kuliko wengine na akawapa baadhi yao vitabu, basi kwa nini wanaomkadhibisha Muhammad -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - wanakanusha yale aliyoteremsha Mwenyezi Mungu juu yake na yale aliyomfadhilisha kwayo ya unabii na Kitabu?