الإسراء
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَقُل لِّعِبَادِى يَقُولُوا۟ ٱلَّتِى هِىَ أَحْسَنُ ۚ إِنَّ ٱلشَّيْطَـٰنَ يَنزَغُ بَيْنَهُمْ ۚ إِنَّ ٱلشَّيْطَـٰنَ كَانَ لِلْإِنسَـٰنِ عَدُوًّا مُّبِينًا ٥٣
{53} Na haya ni katika upole wake kwa waja wake, ambapo aliwaamrisha wawe na maadili mema, vitendo na maneno yenye kuleta furaha duniani na akhera. Akasema, "Na waambie waja wangu waseme yaliyo bora zaidi." Hii ni ya kwamba waseme kila neno yenye kumleta mtu karibu na Mwenyezi Mungu, kama vile kusoma, kufanya dhikri, elimu, kuamrisha mema na kukataza maovu, na kusema kwa uzuri na upole na watu bila ya kujali nyadhifa zao na vyeo vyao, na kwamba ikiwa jambo linazunguka baina ya mambo mawili mazuri, basi ameamrishwa kulipendelea lililo zuri zaidi kati ya mawili hayo ikiwa haiwezekani kufanya uwiyano kati yake, na kauli nzuri ni sababu ya kila tabia nzuri na matendo mema. Kwani mwenye kuutawala ulimi wake, atatawala mambo yake yote. Na kauli yake, “Kwa maana hakika Shetani huchochea ugomvi baina yao." Yaani anafanya bidii kati ya waja ili kuwaharibia dini yao na maisha yao ya kidunia. Na dawa ya hayo ni kwamba wasimtii katika maneno mabaya anayowaitia, na kwamba wawe wapole wao kwa wao, ili akomeke shetani anayechochea ugomvi kati yao. Kwa maana yeye ndiye adui wao wa kweli ambaye wanapaswa kupigana naye. Kwa maana, anawaita ili wawe katika wenza wa Moto. Na ama ndugu zao, hata kama Shetani anapotaka kuchochea kati yao na akafanya bidii ya kuweka uadui kati yao, basi na liwe azimio lao lote ni kujitahidi dhidi ya adui yao huyu, na kuzikomesha nafsi zao ziamrishazo mabaya, ambazo Shetani huingilia humo. Na kwa hayo watakuwa wamemtii Mola wao Mlezi, na mambo yao yatanyooka, na wataongolewa kwenye uongofu wao.