الإسراء
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
أَفَأَصْفَىٰكُمْ رَبُّكُم بِٱلْبَنِينَ وَٱتَّخَذَ مِنَ ٱلْمَلَـٰٓئِكَةِ إِنَـٰثًا ۚ إِنَّكُمْ لَتَقُولُونَ قَوْلًا عَظِيمًا ٤٠
{40} Na hili ni katazo kubwa kwa mwenye kudai kwamba Mwenyezi Mungu amejifanyia mabinti kutoka kwa viumbe wake, akasema, "Je, Mola wenu Mlezi aliwateulia nyinyi wavulana." Yaani, aliwachagulia nyinyi walio bora zaidi na kundi lililo kamili, "naye akawafanya Malaika ni banati zake," ambapo washirikina walidai kwamba Malaika ni binti za Mwenyzi Mungu. "Kwa hakika nyinyi mnasema kauli kubwa" ambayo ndani yake kuna kumfanyia Mwenyezi Mungu ujasiri mkubwa zaidi, ambapo mlimnasibisha na mwana, jambo ambalo linamaanisha kwamba anahitaji kuwa na mwana, na kwamba baadhi ya viumbe hawamhitaji, na tena wakampa Yeye mgao duni zaidi katika migao hiyo miwili, ambao ni wanawake. Ilhali Yeye ndiye aliyewaumba nyinyi na akawateulia wanaume. Basi ametukuka juu kabisa na ambayo madhalimu wanayasema.