انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الإسراء
السورة ١٧

الإسراء

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٣٩

ذَٰلِكَ مِمَّآ أَوْحَىٰٓ إِلَيْكَ رَبُّكَ مِنَ ٱلْحِكْمَةِ ۗ وَلَا تَجْعَلْ مَعَ ٱللَّهِ إِلَـٰهًا ءَاخَرَ فَتُلْقَىٰ فِى جَهَنَّمَ مَلُومًا مَّدْحُورًا ٣٩

{39} "Hayo" ambayo tumeyaelezea na kuyaweza wazi miongoni mwa hukumu hizi kubwa, "ni katika hekima alizokufunulia Mola wako Mlezi." Kwa maana, hekima ni kuamrisha matendo mazuri na tabia nzuri, na kukataza tabia duni na matendo mabaya. Matendo haya yaliyotajwa katika Aya hizi ni katika hekima ya juu ambayo Mola Mlezi wa walimwengu wote alimfunulia bwana wa Mitume wote katika kitabu kitukufu zaidi, ili awaamuru hayo umma bora zaidi. Na hayo ni katika hekima ambayo mwenye kupewa, basi hakika amepewa heri nyingi. Kisha akazihitimisha Aya hizi kwa kukataza kumuabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu kama alivyozifungua kwa hilo, akasema, "Wala usimweke pamoja na Mwenyezi Mungu mungu mwengine, ukaja ukatupwa katika Jahannamu." Yaani, ukadumu humo. Kwa maana, mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu, basi hakika Mwenyezi Mungu ameshamharamishia Pepo, na mahali pake ni Motoni. "Ukilaumiwa na kufurushwa;" yaani, utafuatwa na lawama, na laana, na kashfa kutoka kwa Mwenyezi Mungu, Malaika wake, na watu wote.